Jana, siku ya Ijumaa tarehe 08/07/05, iliisha mikutano ya dola nane zenye uwezo mkubwa wa kiviwanda (G8) iliofanyika Gleneagles, Scotland na Uingereza, mikutano ambayo yalianza 06/07/05. Lilikuwa lengo kuu
la mikutano yao ni maudhui ya Makubaliano ya Kyoto inayohusu usafi wa mazingira kutokamana na uchafu wa moshi unaotoka kutoka viwanda khasa kutoka dola hizi zinazoongoza ulimwengu kiviwanda. Pamoja na hilo lilijadiliwa suala la madeni ya dola fakiri zikiongozwa na dola za kiAfrika.
Ilionekana wazi tangu mwanzo kuzidi tofauti baina ya washiriki katika mikutano, khasa baina ya Amerika na dola nyengine katika maudhui ya mazingira. Hivyo hivyo baina ya Uingereza na Ufaransa kufuatia tofauti zao ziliotokea katika mkutano wa Muungano wa Uropa uliofanyika Brussels (Ubelgiji) mnamo tarehe 16 na 17 mwezi wa sita, 2005 ambalo lengo lake kuu ilikuwa ni kuweka bajeti ya Muungano wa Uropa kisha kudadisi natija ya kura ya maoni juu ya Katiba ya Muungano wa Uropa uliofanyika Ufaransa na Uholanzi.
Kwa hakika mwenye kuchunguza mikutano haya miwili, nayo ni mkutano wa Muungano wa Uropa na mkutano wa dola nane zenye uwezo mkubwa wa kiviwanda, utakuta kuwa mikutano yote mawili yalimalizika bila makubaliano juu ya malengo yaliyokusudiwa. Lakini pamoja na hilo, walitoka na makubaliano ya kuhujumu masuala ya Waislamu na ufafanuzi wa masuala hayo ni kama yafuatayo: -
- Kama tulivyosema kuwa lengo la mkutano wa Muungano wa Uropa ni kuweka bajeti ya Muungano na kudadisi natija ya kura ya maoni iliofanyika Ufaransa na Uholanzi. Amma kuhusu bajeti ya Muungano, ilidhihirika tofauti kali kutoka Uingereza ambao ilikataa kupunguza ruzuku ya kima cha Euro bilioni 4.6 inazopata kutoka Muungano kila mwaka tangu 1984, pamoja na kuwa Uingereza si nchi inayotegemea ukulima kama nyenginezo zikiongozwa na Ufaransa, Ujerumani, Italia, Uhispania na Ureno zinazofaidika na siasa za kusaidia ukulima huku Uingereza ikikosa misaada hiyo. Kadhalika nchi za Uropa (Mashariki) zinazohitaji kukuzwa kimaendeleo. Ikhtilafu hizo ziko wazi baada viongozi kadha wa Muungano kutuhumiana. Waziri mkuu wa Luxembourg alimtuhumu Blair kwa kusema aliharibu mkutano kwa kusisitiza rai yake. Akaona mwenyekiti wa mkutano kuwa mzozo ulichipuka baina ya wale wanaotaka Muungano uwe soko kubwa uliopanuka na baina ya wale wanaotaka Muungano wa kisiasa za dola zilizopo. Hayo yalithibitishwa na Nikolas Dagran, mjuzi wa siasa za Uropa kutoka taasisi ya mafunzo ya kifalme huko London, pale aliposema katika jarida la Al-Hayat tolea la tarehe 1 June kuwa "raia wa Uingereza wanautazama Muungano kama shirika la kiuchumi na sio kama muundo mmoja wa kisiasa, huku akidokeza kuhusu kuwafikiana kwa Amerika na Uingereza katika nyanja hii. Hilo ni kwa sababu Washington yafadhilisha katika upande wa siasa kuamiliana na nchi za bara la Uropa moja moja, na mfano mzuri wa hilo ni suala la Iraq.” Pia alithibitisha waziri mkuu wa Austria ikhtilafu zilizopo katika Muungano yaliyonukuliwa na Reuters mnamo tarehe 9 June: “Tatizo khasa ni kuhusu mali, ufahamu na taswira ya Muungano wa Uropa. Uingereza unapendelea Uropa tofauti inaotegemea zaidi nguvu ya soko …na wanaotaka mfano huu, wao wanawacha nyuma mfano wa kijamii." Hivyo hivyo Chirac alikemea ubinafsi wa baadhi ya nchi huku akimlenga Blair, pale alipozungumza kuhusu kutanguliza uzalendo kuliko maslahi ya Uropa. Pia waziri mkuu wa Ujerumani, Shroeder, na waziri mkuu wa Uholoanzi walimbebesha Blair masuuliya ya kuharibu mkutano. Blair kwa upande wake aliutetea msimamo wa nchi yake wa kukataa kuwacha ruzuku iliotunukiwa Uingereza inayodhamini kupata kwake Euro bilioni 4.6 kutoka bajeti ya Muungano kama badili kwa dola isiotegemea ukulima, kama alivyosema kwa kauli yake: “Ikiwa twataka kumaliza sababu za kupwekeshwa huko, itabidi tumalize sababu zake kwani dhurufu hiyo imeletwa na sababu nyengine” huku akikumbusha kuwa asili mia arobaini ya bajeti ya Uropa imetengwa kufadhili siasa ya Ushirikiano wa Ukulima, zikifaidi dola zinazotegemea ukulima zikiongozwa na Ufaransa. Amma udadisi la suala la kura ya maoni na kudumu katika kuhakikisha natija nzuri katika dola nyenginezo: Hilo limekabiliwa na ukaidi wa baadhi ya dola hali iliyo tatiza mambo badala ya kutengeneza, kwani ilikwamisha suala la kura ya maoni kama ilivyofanya Uingereza au kuiahirisha kama ilivyofanywa Ureno, Udenimaki. Sweden, Czech na Finland. Ni wazi imekuwa nzito au hata kushindikana kukamilisha hatua ya kukubaliwa katiba mwishoni mwa 2006 kama ilivyokubaliwa. Yaani mkutano ulishindwa kwa kila vipimo kwa mujibu wa lengo kuu ya mkutano huo. Ikhtilafu hizo zilichacha baina ya nguzo zake kadha. Pamoja na hayo Muungano uliwafikiana kwa rai moja juu ya swala la Falastin, pale ilipotaja Muungano katika bayana yake: “Utawala wa Falastin kutekeleza kikamilifu majukumu yake katika nyanja ya usalama kwa mujibu wa maazimio ya mkutano wa Sharm al-Sheikh ya kusimamisha mapigano…na Utawala wa Falastin udhihirishe kujitolea kwake katika kupambana na ‘ugaidi’” kana kwamba maFalastini ndio wanaowafanyia uadui mayahudi. Na kana kwamba mayahudi hawakunyakua Falastin pamoja na kuwafanyia uadui wenyeji wake, uadui unaotekeleza mauwaji wa kinyama asubuhi na jioni mpaka ikajumuisha watu, majengo na miti.
- Amma mkutano wa dola zenye nguvu za kiviwanda, lilikuwa lengo lake ni suala la mazingira (Mwafaka wa Kyoto) na kusaidia wenye madeni kwa kusamehe madeni yao. Amma juu ya Mwafaka wa Kyoto ikhtilafu zilibakia hivyo hivyo, kwani Amerika haitaki kuwekewa viwanda vyake (vichafu) vikwazo ili kuweka kikomo kwa moshi unaodhuru na kuchafua mazingira, wakati ambao dola nyenginezo zina lengo hilo. Amma Uingereza, ambayo ni mwenyekiti wa mkutano huu, ni kama ilivyo ada yake; huwafikiana na akili yake ya kutuliza tatizo kwa kubakisha tatizo. Rai ya Blair ni kwa dola chipukizi kiviwanda kupunguza pole pole moshi wa ‘carbon oxide’. Hatua hiyo kwa sasa itasahilishia dola kubwa za kiviwanda, na khasa Amerika, kukubali kurudi katika mazungumzo ya kimataifa kwa sababu ya kubadilika dhurufu! Yaani Blair aigurisha tatizo la kuchafuka mazingira kwa dola chipukizi kiviwanda ili kusahilishia dola kubwa, khasa Amerika, kurudi tu katika mazungumzo juu ya Mwafaka wa Kyoto na sio kuiwafikia. Amma kuhusu maudhui ya ufukara, imekuja maazimio kutekerenya hisia za dola fakiri lakini kiuhakika wataka kufuta deni hizo mukabala wa kuwa na athari juu ya dola hizo fakiri chini ya msamiati tofauti kama mageuzi, demokrasia na haki za kibinadamu… Ni wazi kuwa pindi Washington ilipodokezea suala hili na kulitilia nguvu. halikukusudia lengo hilo ila kwa kadiri kuwa ni fursa ya kupata athari mukabala wa msamaha wa sehemu ya deni. Kuhudhuria kwa maraisi wa benki kuu la dunia na sanduku la fedha la kidunia ni dhihirisho wazi kwa nia mbovu ya kufanya suala la deni ni mlango wa kuziingiza taasisi hizi mbovu. Kwa hakika nia hii ilidhihirika wazi pale alipopendekeza Bush kuhusishwa suala la mageuzi kama njia ya kupata athari. Hivyo hivyo ikhtilafu zilikuwa wazi, bali tuhma zilikuwa wazi, baina ya Uingereza na Ufaransa. Pindi Ufaransa ilipohesabu nishati ya Uingereza katika suala la deni la Afrika kuwa ni nishati bandia na za kirongo kwa sababu lau kama Uingereza kikweli ilitaka kutatua ufukara, ingeunga mkono mwanzo bajeti ya Muungano wa Uropa kukuza dola za Uropa Mashariki ambazo zimejiunga na Muungano hivi karibuni. Na hilo litapatikana kwa Uingereza kuwachia pande lake la pesa chungu nzima ilizokuwa ikipata kutoka bajeti ya Muungano tangu 1984. Ikadhihirika ikhtilafu baina ya dola zenye uwezo mkubwa wa kiviwanda hata baada ya azimio la kufuta deni la bilioni 40, kwani wao walikhtalifiana katika ala za utendaji. Amerika kama ada yake ilifadhilisha kuwekwa makubaliano baina nchi mbili kwa wakati mmoja ili kuwekwa kwa mujibu wake shuruti za kutoa mali pole pole. Amma Uropa, unapendelea makubaliano yanaokusanya nchi nyingi kwa wakati mmoja.
Hivyo ndivyo dola za kiviwanda zilivyobakia na ikhtilafu zao juu ya mambo muhimu mikutanoni lakini, pamoja na hilo, waliwafikiana kuhujumu masuala ya Waislamu kwani wao waliwafikiana katika bayana yao kuunga mkono Utawala wa Falastin katika kupambana na kile wanachokiita ugaidi dhidi ya mayahudi, na kukiri mradi wa dola ya mayahudi ilionyakua Falastin. Wao pia wamewafikiana kuunga mkono serikali ya Iraq ilioko chini ya ukoloni wa mwamerika. Kadhalika waliunga mkono suluhisho zilizo pendekezwa juu ya Darfur zitakazo peleka kujitenga kwake au, kwa ‘hali bora’, kuwa ni utawala wa kimajimbo. Basi ni wazi kuwa mawafikiano juu ya masuala yote hayo ni kuhujumu maslahi ya Waislamu.
Enyi Waislamu!
Nyinyi mwaona dola hizi, na khasa zile za kikoloni na zenye tamaa zinazolenga biladi zetu, hukhtalifiana juu ya kila kitu lakini huwafikiana dhidi yenu. Yaani kuhusu suala la Waislamu, wote huelekea upande mmoja nao ni kubakia masuala ya Waislamu katika mizozo, mafarakano an migawanyiko. Na maeneo yetu yawe ni maeneo ya maslahi kwao wao na kwa mayahudi, na ili wawazue Waislamu kuwa Umma mmoja chini ya dola moja la Al-Khilafa Ar-Rashida, ambalo litarudisha kila kitu mahala pake, kuwarudishia haki wenyewe na kueneza kheri katika kila pembe ya ulimwengu.
Kwa hakika dola za kikafiri za kikoloni, khasa Amerika na Uingereza, zina chuki mbaya kwa Uislamu na Waislamu. Wao mwanzo wanapopata fursa nzuri hudhihirisha chuki yao na zilizofitamana katika miyoyo yao ni makubwa zaidi. Wao husahau ikhtilafu zao ikiwa jambo lahusu Uislamu na Waislamu, kwani pindi milipuko ya London yalipotokea wakati mmoja na mkutano wa dola nane zenye nguvu za kiviwanda wakafichua mtazamo wa chuki wa kimsalaba juu ya Uislamu na Waislamu. Mpaka ikafikia kiwango kuwa kila Muislamu Uingereza hata muingereza asili amekuwa mshukiwa, bali baadhi ya vyama vya kiengereza vimeanza kutangaza wazi wazi kwa “kupiganwa vita vya kimsalaba ili kuwafukuza Waislamu kutoka Uropa.” Kadhalika ilivyoanza kudhihirika visa vya kulipizia kisasi dhidi ya Waislamu, wa kiume na kike, ambao hudhihrisha kujifunga kwao na Uislamu kama wanawake wanovaa hijabu na wanaume waliofuga ndevu, seuze mshambulizi dhidi ya misikiti.
Baada ya tukio la milipuko siku ya Alhamisi 07/07/05, na kabla ya uchunguzi wowote wa kikanuni, bali hata kabla ya kutambuliwa uhakika wa milipuko: Je yametokea kupitia mabomu ya kutegwa au kupita mtu kujitolea mhanga. Tayari zilidhihiri misemo ya kimsalaba ya kichuki, kwani Blair alitoa bayana kwa haraka akiashiria Uislamu na wengineo pia walituhumu Uislamu kama dini mbovu ya kinyama…hivi ndivyo ilivyodhihirika chuki yao ya kimsalaba dhidi ya Uislamu na Waislamu. Wao wanajua wazi kuwa milipuko mengi husababishwa na watu wao wenye siasa kali walae hawakuwaita kama wanvyowaita Waislamu, wala hawakusubutu kuzitaja kwa uovu dini yao, hadhara yao au maadili yao kwa jina lisilo laiki, bali maneno yao hukoma juu ya wahusika tu.
Enyi Waislamu!
Pamoja na kuwa sisi Hizb ut-Tahrir hatuhalalishi kuuwawa kwa raia wala hatukubali kuwadhuru watu wa kikawaida wasiokuwa wapiganaji, na sisi twatofautisha baina ya eneo la mapigano katika uwanja wa vita kati ya majeshi, na baina ya mshambulizi ndani ya miji. Pale majeshi yanapo pigana wakaua au kuuliwa, jeshi linalopigana katika nia ya Allah ndio wenye ujira na ushindi. Amma katika miji na baina ya raia jambo, hilo ni tofauti wala si sahihi wala halifai. Uislamu ulitoa mfano mzuri katika vita vyake na muamala wake katika ukombozi wa kheri ambao hufanywa kueneza uadilifu katika kila pembe ya ulimwengu na ushahidi wa hilo ni vitendo vya Salahuddin pale alipoikomboa Al-Quds kutoka majeshi ya kimsalaba. Wakati aliposhinda katika uwanja wa vita na kuingia Al-Quds, yeye hakumwaga damu wala kumuua mteka hata mmoja; ihali lilipoingia jeshi la msalaba humo lilimwaga damu za Waislamu ndani ya Mskiti Al-Aqsa hadi damu kumiminika kiasi cha magoti kama walivyonukulu wanahistoria. Huu ndio Uislamu, hadhara yake na maadili yake na yale ndiyo chuki, hadhara na maadili ya majeshi ya kimsalaba.
Twasema, pamoja na kuwa sisi Hizb ut-Tahrir ni dhidi ya vitendo vya milipuko mijijini wala hatuzihalalishi, lakini twauliza: Kwa nini wamagharibi hutazama maiti zao kwa mtazamo mmoja na hutazama maiti ya Waislamu kwa mtazamo mwengine? Kwani Waislamu waliouliwa Falastin, Iraq, Afghanistan, Chechniya, Kashmir, Filipino na wanaouliwa huku na huku na damu zao kumwagwa kwa uadui na dhulma asubuhi na jioni na dola za mayahudi, Amerika, Uingereza, Urusi, India, Thailand, Ufilipino na kwa mikono ya kila twaghuti wa kila jinsi. Kwa nini hawa waliouliwa kidhulma na kwa uadui huhesabiwa na mjumuiko wa dola nane zenye nguvu kiviwanda kuwa waliuliwa katika hali ya kulinda nafsi! Amma wakiuliwa waamerika, waingereza, wahindi na wengineo husimama dunia nzima kwa ajili yao wala halikai? Kwani hawa wamagharibi na mayahudi hawataraji kuwa mauwaji ya Waislamu ya kinyama yatazalisha jawabu kali kutoka kwa Waislamu?
Kwa nini hawataraji kuwa kuvunja heshima, kunajisi Mswahafu na maeneo matukufu, kutenda uovu wa kinyama unaofanywa katika biladi za Waislamu zilizonyakuliwa kama Falastin, Iraq, Afghanistan, Kashmir, Chechniya na nyenginezo, kwa nini hawakutazamia kuwa mambo hayo yanaweza kuwasukuma baadhi ya watu msukumo wa kulipizia kisasi kwa sababu ya kuuwawa kidhulma; kwa nini hawakutarajia hilo?
Kwa nini hawatatui tatizo kwa kukomesha uadui wao dhidi ya Waislamu na kujizuia kumwaga damu za Waislamu? Kwa nini wao hawaangalii chanzo cha matatizo na kulimaliza, badala ya kuangalia athari na sababu za athari?
Enyi Waislamu!
Ni wazi kuwa makafiri wakoloni hukhtalifiana sana katika mikutano yao, lakini ikiwa juu ya kuuhujumu Uislamu na Waislamu wao hujumuika juu yake. Na wao pindi wanapopata fursa hudhirisha wazi wazi uadui wao na chuki zao. Yaliyofuatia milipuko ya London katika bayana za chuki kutoka Bush, Blair, Putin, Chirac, Shroeder na Berlusconi—na hata kutoka Ujapani, Canada na kutoka mbali hadi Australia—yote hayo hufichua chuki walionao dhidi ya Uislamu na Waislamu hata kabla kubainika uchunguzi au kuhakikishwa ukweli.
Enyi Waislamu!
Sisi twadiriki kuwa vitendo hivi vya ulipuaji vya miji na watu havitatui tatizo la uadui wa makafiri dhidi ya Waislamu licha ya kuwa halisihi kufanywa ndani ya miji wala halifai kufanyiwa raia wa kikawaida asiekuwa mpiganaji. Litakalo tatua tatizo ni kurudisha dola la Waislamu, Al-Khilafa Ar-Rashida, ambalo litarudisha Umma mahali ambapo Allah atairidhia nao ni Umma bora uliojitokeza kwa watu. Litarudisha izza na fahari yake, na litakata mkono wa kila kafiri mkoloni atakao unyoshea kwa Waislamu. Litauhifadhi Uislamu, heshima za Waislamu na maeneo matukufu, na kukomboa maeneo na kueneza kheri katika kila pembe ya ulimwengu.
Hizb ut-Tahrir yaendelea njia hii wala haifanyi matendo ya ki-mada wale haioni kuwa ni tatuo sahihi; wala haihalalishi kuuliwa raia wa kawaida wala kuwadhuru watu wa kawaida. Lakini pamoja na hilo yaona kuwa kuvuka mipaka kwa dola kubwa katika kumwaga damu za Waislamu, heshima zao, na kunajisi maeneo yao matukufu ndio sababu ya kihakika inayosababisha hali ya kulipizia kisasi. Lau dola hizo kubwa zingetaka kukomesha vitendo hivi kikweli, zingeanza kuyafikiri masuala tuliyoyauliza hivi punde; lakini sisi twadiriki kwamba kiburi za dola hizi itazizuia kufikiri kwa njia ya sawa.
Enyi Waislamu!
Kwa hakika ulimwengu umekorogeka, na dola kubwa zimekorogeka zaidi; bali wao ndio sababu za mkorogano huu. Uislamu ndio pekee unaoweza kuongoza ulimwengu, kuukomboa na kueneza kheri katika kila pembe ya ulimwengu. Yote hayo huanza kwa kufanya kazi pamoja na Hizb ut-Tahrir kwa bidii na ikhlasi ili kurudisha maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha dola la Al-Khilafa Ar-Rashida. Asema Ta’ala:
هَذَا بَلاَغٌ لِلنَّاسِ وَلِيُنذَرُوا بِهِ وَلِيَعْلَمُوا أَنَّمَا هُوَ إِلَهٌ وَاحِدٌ وَلِيَذَّكَّرَ أُوْلُوا الأَلْبَابِ
“Hayo yatosha (kuwa mawaidha) kwa watu ili waonywe kwayo na wapate kujua kuwa yeye ni Mungu mmoja tu, na ili wenye akili wakumbuke” [TMQ Ibrahim:52]