Friday, July 22, 2011

NYINYI NI UMMAH BORA KULIKO UMMAH ZOTE

Kwenu Ndugu Waisilam!

Allah (swt) amekueleezeni kuwa nyinyi ni Umma bora kuliko umma zote miongoni mwa binaadam. Hii ni kwa sababu munauzunguza ukweli na kukabiliana na uzito kwa sababu ya kufanya hivyo.
Uvamiaji na utawaliji wa Afaghastani na Iraq imesababisha mengi katika jamii zetu za Kiisilam na kuwa mstari wa mbele katika kuuzungumza ukolani unaofanywa na nchi za Magharibi, dhuluma dhidi ya Umma wetu huu wa Kiislam, uuwaji na ukandamizaji wa kaka zetu na dada zetu na sera za nje za kikatili (foreign policy) za Uengereza na Marekani. Kuyazungumza yote haya kwa uwazi si makosa (crime) bali ni moja ya wajibu mkubwa wa kila Muisilam mwanaume na mwanamke.

Mtume (saw) ametukumbusha umuhimu wa kuzungumza ukweli dhidi ya uovu pale aliposema :

والذي نفسي بيده لتأمرن با لمعروف ولتنهون عن المنكرأو ليوشكن الله أن يبعث عليكم عقا با من عنده ثم لتدعنه فلا يستجاب لكم

“Naapa kwa yule ambaye maisha yangu yapo mikononi mwake, Ni lazima muaamrishe mema na mukataze mabaya, laa sivyo Allah (swt) atakuleteeni adhabu kubwa kutoka kwake na nyinyi mtasali kwa kumuomba akusaidieni lakini Yeye (Allah) hatokujibuni dua zenu”

Ikiwa Umma wetu huu hauto uzungumza ukweli kwa uwazi na kubakia kimya kwa yanayowafikia Waisilamu duniani, ni nani mwengine atauzungumza? Leo Dunia nzima imenyamaza kimya kwa yanayowafikia umma wetu huu. Mauwaji ya kigaidi dhidi ya Waisilamu 120,000 Iraqi ni hasara isiokuwa muhimu (collateral damage) ambao haisabaki. Mauaji ya Andijan – Uzbekistan yameficha katika vyombo vya habari kwa watu kuyaona. Wanawake wanaolia kutoka katika mahandaki ya Chechnya hakuna anayesikia vilio vyao. Hakuna sala wala dua kwa watoto wa Afghanistan wala hakuna buku la maombolezi kwa watoto wa Iraq. Hii yote ni kwa sababu thamani ya maisha si sawa kwa wote.

Bila ya shaka maisha ya binaadam yeyote yatakayo tolewa kinyume na sheria ni uovu (Munkar), ikiwa ni London au Baghdad, lakini vipi maisha ya watu wanaouliwa na majeshi ya Uengereza na Marekani yanakubalika na viongozi wa Magharibi kuwa ni gharama inayokubalika (price woth paying)? Hakuna anaye uliza, ni kitu gani alichokuwanacho kijana ambaye anamaisha ya baadaye kuvaa guo la jeshi na kuuliwa kwa jina la Queen na nchi yake. Hakuna anaye uliza kuwa Uisilam, ambao unakandamizwa katika vyombo vya habari na kusema kuwa ni dini ya fujo haikuwahi kutuma jeshi kuua kwa ajili ya mafuta (oil) na faida ya mashirika makubwa.

Hakuna atakae uliza haya leo ikiwa midomo na sauti zetu zimenyamaza. Sauti ambayo inauliza maswali juu ya yale ambayo vyombo vya habari vimenyamazia kimya. Sauti ambayo inazungumza kwa niaba ya wanyoge na wanaodhulumiwa. Sauti ambayo inalingani Haqi ya Allah (swt).

Ndugu Waisilam!
Kuzugumza ukweli si kosa la jinai, si ugaidi (terrorism) wala si extremism. Kuzungumza ukweli ni wajibu wa kisheria kutoka kwa Allah (swt). Hivyo timizeni wajibu wenu huu kwa mazungumzo ya hikma na mijadala ya busara.

Mtume wetu Muhammad (saw) aliuchukuwa wajibu huu kwa kipindi cha miaka 13 Makka bila ya kutumia nguvu na fujo katika kukumbana na madhalimu wa Quraysh, amabo walitumi uenezaji wa habari mbovu dhidi ya Mtume na Waisilam, mateso, unyanyasaji na njaa. Aliporudi kutokea Taif ambapo alipigwa mawe na watoto wa mji huo, Mtume alinyanyua mikono na kuomba dua kwa Allah (swt):

“Ewe Mola wangu! Ni kwako naleta malalamiko yangu ya unyonge, uhaba wa uwezo na udogo mbele za watu. Ewe Mwingi wa Rehema! Wewe ni Bwana wa wanyonge na Wewe ni Mola wangu. Ni kwa nani utanisitiri mimi? Je, ni kwa yule aliyenitumia kwa ubaya au kwa adui uliempa utawala dhidi yangu?”
Hivyo ndugu Waisilamu! Endeleeni kuuzungumza ukweli, kwani ni Allah (swt) ndie atakae kusaidieni na kukupeni sehumu ilio bora zaidi.
-
إنَا لَنَنصُُُرُرُسُلََنَا وَالَذِينَ ءآمنُوافِى الحَيَوةََ الدُُُُُنيَا وَيَومَ يَقُومُ الأَشهدُ
-
“Bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume yetu na wale walioamini katika maisha ya dunia na siku watakapo simama mashahidi (kushuhudia amali za viumbe)” [Ghafir : 51]