Wanasiasa wa kimataifa na watunga sera wa nchi zenye nguvu ambazo ndizo zinazoongoza dunia ya leo wakianza kujadili juu ya jambo katika maongezi yao, ni muhimu kufahamu kuwa jambo hilo lina umuhimu
sana kujadiliwa. Suala la Khilafah “Caliphate” limo katika ulimi na mazungumzo ya viongozi wa juu wa serikali ya Mareikani, Uingereza, Ulaya na nchi zinginezo za Mashariki ya kati “Middel east” na Asia.
Eric Edelman, chini ya baraza la secretary wa ulinzi Marekani alisema katika bayana yake kuhusiana na suala la Ukhalifah “Caliphate” aliyoitoa mwezi wa November na December 2005 katika kikao cha mashauri ya mambo ya nje kuwa “..maenedeleo ya Iraq yatakuwa ni ya kuwajenga magaidi na kupanua uwezo wao wa kusimamisha Ukhalifah au utakuwa ni kipigo kikali na kufeli kwao.”
Secretary wa Ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld alisema pia katika bayana yake aliyoitoa tarehe 05/12/2005 mjini Washington kuwa “Iraq itakuwa ndio mzizi wa uongozi mpya wa Khilafah “new Islamic Caliphate” na kupanuka Mashariki ya kati yote “Middel East” ambao utatishia serikali zote za Ulaya, Afrika na Asia. Hii ndio plani yao walioisema wenyewe. Tutafanya makosa makubwa sana kama tutafeli kusikiliza na kusoma.” Pia alirejea kulisema neno hilo siku tatu baada kwa mara nyingine tena mnamo tarehe 08/12/2005 katika mahujiano yake na PBS.
Kabla ya kusemwa hayo, Stephen Hadley, mshauri wa usalama wa taifa alirejea kuhusiana na Ukhalifah “Caliphate” mwezi wa kumi October 2005 katika bayana yake mjini New York na Los Angeles wakati jenerali mkuu wa jeshi la Marekani katika Mashariki ya kati “Middel East” John Abizaid alisema “..watajaribu kusimamisha utawala wa Khilafah “Caliphate” katika bara zima la Waisilamu.”
Ama kuhusiana na Raisi George Bush, ijapokuwa hajatumia neno hilo kipindi hicho lakini aliuelezea Ukhalifah kuwa ni “utawala mmoja wa "empire" ambao utatawala kutoka Indonesia hadi Spain.”
Suala ni kuwa ni kitu gani kilichosababisha uongozi wa Marekani kuanza kulitumia neno hili la Caliphate “Khilafah” kuwa ni jambo muhimu la kulijadili katika ufunguzi wa mazungumzo yao? Si jambo ambalo linahusiana na Al-Qaida au ugaidi kama Marekani anavyodai katika “vita dhidi ya Ugaidi” (war on terror), anataka ulimwengu waamini. Bali jambo hili la kurudi kwa Ukhalifha ni muhimu sana kwa wengi wa wanasiasa wa Magaribi na wahuduma wastaafu wa serikali na wanalitilia uzito katika kulidhibiti kama ilivyokuwa wakati wa McCarthyism ambapo Marekani aliamua kupambana na Ukominist miaka ya 1960 wakati wa vita baridi “Cold War”.
Uwazi ni kuwa hamu na shauku kubwa ya Umma wa Kiisilamu wa kurudi tena utawala wa Kiislam “Khilafah” inakuwa siku hadi siku ulimwenguni. Ni ushahidi tosha pia Marekani na nchi zingine za Kibepari na vibaraka vyao walioko nchi za Waisilamu wamehisi ukuwaji na ongezeko kubwa la matumaini hayo ya Umma wa Waisilamu, na ongezeko la harakati za kisiasa za Kisilam katika kurudisha tena utawala wao huo wa Khilafah. Hivyo ilikuwa hakuna budi na ni wajibu wa Marekani kushambulia fikra hiyo ya Mfumo wa Utawala wa Kiisilam “Khilafah” kwa lengo la kuwaweka mbali Waisilam na harakati hizo na kuwaonya watu wao na jambo hilo la Ukhalifah “Caliphate”.
Waisilam ni lazima walichukuwe ndani ya nyoyo zao jambo hili kwani ni sehemu ya imani na itikadi ya Kiislam. Ni wajibu wao Waisilam kulijadili na kulileta katika mazungumzo na mijadala jambo hili la Ukhalifah. Bila ya shaka wakati umefikia kuwa jambo hili si ndoto tena kurudi kwake ulimwenguni bali uhakika wa kuwa lipo njiani kutufikia na linazidi kutikisa Utawala wa viongozi Madhalimu wa Mashariki na Magharibi.
Waisilam pia ni lazima watambue kuwa mjadala unaofanyika katika Uongozi wa nchi za Magharibi inaashiria kuwa wametambua kurudi kwa Ukhalifah na wanafanyakazi ya kudhorotesha ufikaji wake na si kuzuia tena. Kwani kuwasili kwake sasa ni suala la wakati na si uwezekano tena.
Tangu kuondoshwa kwa Ukhilafah mnamo mwaka 1924, wajibu wa kufanyakazi ya kurudisha Utawala wa Kiisilam “Ukhalifah” umekuwa ndio wajibu wa kufa na kupona kwa waisilam kama ilivyo kuwa haramu kwa Waisilam kuishi hata kwa saa moja bila ya kuewepo sheria zake Allah (sat). Na Inshaallah kusimama kwake sasa imekuwa ni suala la wakati gani utatangazwa kuwasili kwake duniani kwa mara nyingine tena.
Hudhayfah ibn Al-Yaman amesimulia kutoka kwa Mtume (saw) kasema kuwa :
...ثم تكون الخلافة على منها ج النبوة
“…kisha utarejea tena Ukhalifah Rashidah kwa kupitia njia ya Bwana Mtume, kisha akanyamaza.” (Musnad Imam Ahmad 4/273).