Tuesday, October 24, 2006

WAJIBU WA KUWEPO KWA KUNDI ILI KURUDISHA DOLA LA KIISILAMU



Mnamo tarehe 3rd March, 1924 jasusi Mustafa Kamal Ataturk (Uturuki), baada ya kupanga mipango yake ya kuuwangusha utawala wa kiisilamu (Khilafah), alitangaza katika Baraza la Taifa kuwa utawala wa
Kiisilamu (Khilafah) lazima uondoshwe. Siku hiyo hiyo aliamrisha ya kuwa Khalifah Abd al-Majid bin Abd al-Azeez amabye alikuwa ni Khalifah wa mwisho wa umma wa Waisilamu aondoshwe nchini (Uturuki) na
kwenda Switzerland. Wakati huo huo ilikuwa ni wajibu kwa Waisilamu kujiunga pamoja na kuchukuwa jukumu la kufa na kupona juu ya kuurudisha utawala wa Khilafah kama alivyo faradhisha Allah (sw). Lakini kutokana na udhaifu wa Waisilamu juu ya ufahamu wao wa Uisilamu na kwa sababu ya udhaifu wa hofu yao kwa Allah (sw) katika nyoyo zao hawakutilia manani sana kutokana na vitisho vilivyofanywa dhidi yao na Mustafa Kamal na nchi za Magharibi. Walinyamazia kimya upinduliwaji wa Khilafah, ugawanishwaji wa ardhi ya Waisilamu na kufanywa nchi mbali mbali na walinyamazia kimya juu ya sheria zilizotungwa na binaadamu katika maisha yao badala ya sheria za Allah (sw). Walisahau maneno ya Mtume (saw)

ومن ما ت وليس في عنقيه بيع ما ت ميتة جهلية

Yeyote atakaye kufa bila ya kuwepo Bayah (utiifu kwa Khalifah) juu ya shingo yake, atakuwa amekufa kifo cha kijahiliya (kabla ya Usilamu)”

Leo Wasilamu wanaweza kuepukana na kaburi hili la dhambi ambalo limeelezewa kwa uwazi na bwana Mtume (saw) kama ni kifo cha Ujahiliyyah na kuondosha unyanywasaji unaofanywa dhidi ya umma huu kutokana na kuangushwa kwa Ukhailifah. Waisilamu lazima wafuate njia ya Mtume (saw) ambayo ni hukum ya Allah (sw) katika kurudisha mfumo wa maisha ya Kiisilamu na kusimamisha tena Utawala wa Kiisilamu (Khilafah) na kumchaguwa Khalifah wao. Na njia hii imetokana na maandishi ya sheria (Qur-aan) na seerah ya Mtume (saw) ambayo inawalazimikia Waisilamu kuanzisha kundi la watu ambalo litakalofanya kazi ya kurudisha tena Ukhalifah kufuatana na maneno yake Allah (sw):

ولتكن منكم أمة يدعون إلى الخير ويأمرون بالمعروف وينهون عن المنكر وأولئك هم المفلحون

Na liwepo katika nyinyi kundi (Chama) la watu wanaolingania kheyri (Uisilamu) na wanaoamrisha mema (Maaruf) na wanaokataza maovu (Munkar). Nao hao ndio watakaotengenekewa (watakaofaulu)”
3;104.

Hii ni amri kutoka kwa Allah (sw) kwa Waisilamu kuanzisha kundi la watu au chama kutokana miongoni mwao ambalo litalingania Kheyri (Uisilamu), kuamrisha mema (Maaruf) na kukataza mabaya (Munkar). Kama watafanya hivyo watakuwa miongoni mwa waliofaulu na kupata Radhi na Malipo ya Allah (sw). Amri katika aya hii juu ya kuwepo kwa kundi hilo la watu ni moja ya fardhi (wajibu) kwa sababu kuamrisha mema na kukataza mabaya ni wajibu wa lazima, nao umeambatanishwa na kuwepo kwa kundi la watu ili jukumu hilo lifanywe na (Falah) kufaulu inategemea kwa utendaji wa wajibu huo.

Wajibu umekuja moja kwa moja kwa kuwepo kwa kundi la watu au chama miongoni mwa Waisilamu ambalo litasimamia na kutenda kazi mbili. Kwanza : Kulingania Kheyr nayo ni Uisilamu wote na Pili ni kuamrisha mema (Maaruf) na kukataza mabaya (Munkar). Ijapokuwa ni lazima kwa kila mmoja katika Waisilamu na kwa utawala kutekeleza wajibu hizo mbili, lakini kwa kila mmoja kutekeleza fardhi hii peke yake atakuwa yupo nje ya kundi alilolizungumzia Allah (sw) hususan kwa kutokuwepo kwa nchi ya Waisilamu na Khalifah. Kwa hivyo haitoondosha kosa (dhambi) ya kuwepo kwa kundi la Waisilamu. Kwa hivyo kulingania Usilamu, kuamrisha mema (Maaruf) na kukataza mabaya (Munkar) ni Fardhi, vile vile kuanzisha kundi ambalo lina mpangilio maalum (Structures) kwa lengo hili itakuwa ni Fardhi.

Kuwepo kwa kundi au chama mpaka likaitwa “Umma” au “Jamaa” ni lazima litimize masharti mawili. Kwanza, lazima kuwepo na muungano ambao unaunganisha kundi zima na kuwa umbile moja. Muungano huo lazima ujengeke kutokana na Aya ambayo ni Ulinganifu wa Uisilamu (Dawah ilal-Islam), kuamrisha mema (maaruf) an kukataza mabaya (munkar) ambayo yenyewe ni fikra ya Kiislamu (Fikrat ul-Islaamiya) inamaana ya itikadi (Imani) ya Kiisilamu (A’qeedat ul- Islaam), fikra, sheria na uchambuzi wa mawazo ambayo yamejengeka katika misingi ya Itikadi (Iman) hiyo ambayo ni muhimu kwa walinganiaji au wafuasi katika kutekeleza wajibu huo. Pili, ni kuwepo kwa kiongozi (Ameer) wa Kundi au chama hicho ambaye utiifu kwake ni lazima katika jukumu ambalo amechaguliwa kuliongoza kwa kutokana na ushahidi wa maneno ya Mtume (saw) “ Hairuhisiwi kwa watu watatu kuwepo mahala bila ya kumchaguwa mmoja wao kuwa ni kiongozi (Ameer) wao". Kwa hivyo Kundi au Chama ambacho kinachotakiwa na Sheria ya Allah (sw) kulingania wito wa Uisilamu, kuamrisha mema na kukataza maovu lazima lichanganye mambo mawili pamoja, ambayo ni : Fikra za Kiisilamu na Kiongozi (Ameer) ambaye utiifu kwake ni wajibu.

Ulinganiaji juu ya Uisilamu inalazimisha kulingania na kufanya kazi juu ya kurudisha sheria zote za Kiisilamu katika matendo yote ya kimaisha kama kumkata mkono mwizi, kumpiga bakora mzinifu, kuondosha riba kufikisha wito wa Uisilamu kwa Dawa na Jihad na kuangalia matakwa (maisha) ya Umma kwa kufuata fikra na njia ya Kiisilamu i.e Itikadi (Aqeeda) na suluhisho linalotokana katika Itikadi (Aqeeda) hiyo. Kama ilivyo wajibu wa sheria hizi za Kiisilamu na wajibu wa Utawala wa Kiisilamu. Usimamishaji wa Utawala huu ambao unawajibika kuzitekeleza sheria hizo kwa niaba ya Waisilamu wote ni Fardhi ambayo inatokana na msingi wa sheria “Ma laa yamutimm al- wajib illa bihi fahuwa wajib” (Chochote kinacho kamilisha wajibu nacho pia ni wajibu).

Uanzishaji wa kundi hilo au chama hicho ni wajibu wa kutoshelizana (Fardh al- Kifayya). Kama baadhi ya Waisilamu wataanzisha kundi hilo au chama hicho ambacho kitatimiza misingi yote ya sheria ya Kiisilamu hapo itakuwa dhambi ya kuwepo kwa kundi hilo au chama hicho itakuwa imeondoka, lakini dhambi ya kutofanya kazi ya kusimamisha Utawala wa Kiisilamu haito ondoka. Kundi hilo au Chama hicho kufanya kazi ya kulingania Uisilamu na kuamrisha mema (Maaruf) na kukataza mabaya (Munkar), katika mazingira haya ambayo hakuna Utawala wa Kiisilamu unaotawala kwa sheria alizotuteremshia Allah (sw) na hakuna upiganiaji (Jihad) katika njia ya Allah (sw) kufikisha wito wa Uisilamu duniani, inaifanya kazi ya kusimamisha Utawala huu na kumteua Khalifah wa Waisilamu wote kuwa ndio lengo kuu la kundi au chama hicho. Kwa hivyo kujiunga na Kundi au Chama hicho kinachofanya kazi hiyo ni lazima (Fardh) kwa Waisilamu mpaka Utawala wa Kiislamu usimamishwe na Kiongozi (Khalifah) wa Waisilamu ameteuliwa. Kila ambaye anawajibishwa na sheria (Fardhi) hii (Mukallaf) atakuwa makosani (mwenye dhambi) kama hatoifanya fardhi hii na kufeli kufanya fardhi hii pia ni dhambi.

Kuwepo zaidi ya Kundi au Chama kimoja, imetokana na neno katika Aya tulioizungumzia mwanzo, na imeruhusiwa. Hairuhusiwi kukataza kwa kuwepo makundi au chama zaidi ya kimoja kwa sababu kufanya hivyo ni sawa sawa na kuzuia utendaji wa Fardhi hiyo. Neno “Umma” limetajwa katika Aya i.e. Kundi au Chama ni neno la ujumla ambalo halizungumzii kundi au chama kimoja. Hii ni sawa sawa na maneno ya bwana Mtume (saw)

من رء منكم منكر
Yeyote atakaye uona Uwovu (Munkar)”

Munkar uliokusudiwa hapo si munkari mmoja bali ni munkar zote. Kundi au Chama haitajii ruhusa au kibali kutoka kwa kiongozi ili kuwepo kwake. Kwa upande mwingine inaifanya Fardhi hii kuwa inategemea ruhusa ya kiongozi na kuwa hivyo ni Haramu kwa sababu kutimiza Fardhi kama swala, Hajii, kuwanzisha kwa Kundi au Chama au kufanya kazi pamoja na Kundi hilo au Chama hicho ni utiifu wa Amri ya Allah (sw). Kumtii kiongozi kwa kuacha kufanya Fardhi ili kumtii Allah (sw) ni Haramu na ni dhambi kubwa. Mtume wa Mwenyenzi Mungu (saw) amesema kuwa
لاطا عة الخلق في معصيتي الخا لق

Hakuna utiifu juu ya kiumbe (makhlooq) kwa kumuasi Muumba (Al-Khaaliq )”.

Kwa hivyo kuanzisha Kundi au Chama na Chama cha Kisiasa katika misingi ya Kiisilamu haihitajii ruhusa au kibali kutoka kwa kiongozi au serikalini.

Enyi Waisilamu !!

Tunakulinganieni kuunda au kujiunga na Kundi au Chama kilicho na mpangilio katika misingi ya Uisilamu, kusimamisha Utawala wa Kiisilamu (Khilafah) ambao utawaunganisha Umma wa Kiisilamu chini ya Uongozi mmoja ambao mtaupa kiapo chenu cha utiifu (Ba’ya) kwa kuwaongoza kwa Kitabu cha Allah (swt) (Qur-aan) na mwenendo wa bwana Mtume (saw) Sunnah, hivyo kusimamisha sheria alizoziteremsha Allah (swt) na kuwaongoza katika uwanja wa Jihadi na shahid. Hivyo ubora na utukufu wenu urudi tena. Nanyi mufikishe Uongofu na Mwangaza (Noor) kwa viumbe vyote na kuwatowa katika upotevu na kiza (dhalala), hivyo nayi mupate Radhi nzuri za Mola wenu Allah (swt).

وإن تتولوا يستبدل قوما غيركم ثم لا يكونوا أمثلكم

Na kama mkirudi nyuma(mkaupua mgongo Uisilamu, Mwenyezi Mungu) ataleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi (Watakuwa bora).” (47:38).