Ni nini Hizb ut-Tahrir?
Hizb ut-Tahrir ni chama cha kisiasa cha Kiislam kilichopo duniani kote tangu kilipoanzishwa mwaka 1953 chini ya uongozi wa muanzilishi, mwanachuoni (Alim), mwenye kufikiria, mwanasiasa na aliye kuwa hakimu katika mahkama ya Al-Quds (jerusalem) Mujtahid sheikh Taqiuddin an-Nabhani.
Katika nchi za kiisilam, Hizb ut-Tahrir inafanya shughuli zake katika ngazi mbalimbali za jamii ili kuwarejasha katika mfumo wa maisha wa kiisilam chini ya kivuli cha uongozi wa Khilafah.
Katika nchi za Magharibi, Hizb ut-Tahrir inafanya kazi ya kuwalingania jamii ya Waisilam ili waishi kwa kufuata sheria za Kiisilam, kifikra na kivitendo na kuhifadhi utambulisho wao wa Uisilam. Hizb ut-Tahrir pia inafanya kazi na jamii ya Waisilam waliopo magharibi kwa kuwakumbusha juu ya kulingania wito huu wa kurudishwa kwa uongozi wa Kiisilam (Khilafah) na uunganishaji wa umma wa Kiisilam duniani. Chama kinafanya kazi ya kujenga ufahmu mzuri wa Uisilam kwa jamii ya magharibi kwa kujadiliana na wanazuoni, wanasiasa, wasomi na watunga sera nchi hizo.
Kwa nini Hizb ut-Tahrir inajiita kuwa ni chama cha kisiasa cha Kiisilam?
Si kama kawaida za vyam vya kisekula (utengenishaji wa dini na siasa), katika Uisilam hakuna tofauti baina ya dini na siasa.
Harakati zinazofanywa na Hizb ut-Tahrir ni za kisiasa, kwa sababu lengo la chama ni kuaangalia masilahi ya watu kwa kufuata sheria za Allah (swt) amabzo ni suluhu za matatizo ya maisha ya watu. Mtazamo wa Uisilam juu ya siasa ni kuchunga mahitaji ya watu kwa kufuata sheria za Kiisilam.
Ni ipi njia ya Hizb ut-Tahrir ya kuleta mabadiliko?
Hizb ut-Tahrir inafuata mwenendo aliokuja nao Mtume Muhammad (saw) uliosimamisha utawala wa Kiislam wa mwanzo Madina. Harakti za Mtume Muhammad (saw) za kusimamisha utawala wa Kiisilam zilikuwa ni za mapambano ya kifikra na hoja katika uwanda wa kisiasa. Alianzisha nchi ya Kiisilam bila ya kufanya harakati za fujo na mapigano au ugaidi. Alifanya kazi ya kujenga mawazo katika jamii juu ya Uisilam na kuwakabili wanasiasa, wafanya biashara, watu wa kawaida, masikini na matajiri, na wasomi wa wakati ule kwa hoja za Kiisilam. Ijapo kuwa waliteswa, kuzuiwa chakula na kupigwa Mtume Muhammad (saw) na wafuasi wake wa mwanzo hawakupigana na jamii hiyo ya kikafiri.
Chama kinafuata kwa makini sana njia hiyo ya mapambano ya kifikra na hoja katika harakati za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kielimu kwa sababu tunaamini ya kuwa huu ndio mwenendo uliosawa na wa kweli na wenye matokeo makubwa katika kupelekea kwa kurudi kwa utawala wa Khilafah. Kwa hivyo chama kipo makini na kinafanya kazi sana katika kujenga fikra za sahihi za Kiislam, ufahamu na hoja zake za kisiasa katika jamii yote ya Waisialm ilikupambana na fikra potefu zilizopo katika jamii.
Chama kinawakilisha Uisilam kama ni mfumo kamili wa maisha ambao unauwezo wa kuongoza nchi na jamii. Pia kinaelezea mtazamo wake katika mambo yote ya ksiasa yanayotokea duniani kwa mtazamo wa Uisilam.
Chama kinaweka wazi fikra zake kwa kujadiliana na mkusanyiko wa watu, darsa ndogo, hutuba, mihadhara na usambazaji wa karatasi (leaflet), uchapishaji wa vitabu na majarida na mtandao (internet).
Njia ya chama ya kuleta mabadiliko imeeleziwa kwa kirefu katika kitabu kiitwacho “The methodology of Hizb ut-Tahrir for change”.
Ni wapi Hizb ut-Tahrir kinafanya harakati zake?
Chama kinafanya harakati zake Ulaya (Europe) nzima, Central Asia, Afrika, Middle East, Bara Hindi, Austaralia na Marekani.
Je, Hizb ut-Tahrir inaunga mkono fujo (ugaidi), au inahimasisha ugaidi?
Hizb ut-Tahrir inaamini ya kuwa mabadiliko tunayo yataka ni lazima yanaanzie katika kubadilisha fikra za watu, hatukubali kuwa mabadiliko yalazimishwe kwa watu au jamii kwa njia ya mapigano au ugaidi. Hivyo Hizb ut-Tahrir hailinganii wala kushiriki katika harakati za mapigano au ugaidi. Chama kimejizatiti na kufungamana kwa kufuata sheria ya Kiislam katika harakati zake zote za ulinganifu (dawa). Ni fikra na hoja za kisiasa ambazo tunataka kubadilisha katika mawazo ya watu ili kuleta majadiliano. Tunafahamu kuwa Uisilam umekataza fujo au mapigano dhidi ya uongozi ili kuwa ndio njia ya kuleta mabadiliko ya uongozi wa Kiislam.
Habari nyngi zimeandikwa na kutolewa na vyombo mbali mbali vya habari kama: Reuters, Itar-Tass, Pravda, AFR, Al-Hayat, Ap na RFERL kwa uchache tu ambavyo vimeelezea kwa uwazi ya kuwa Hizb ut-Tahrir si chama cha fujo ambacho kinapinga kabisa mapigano na ugaidi kuwa ndio mwenendo.
Je, Hizb ut-Tahrir ni extremist?
Vyama ambavyo ni extremist vinatumia hofu za watu na hoja ambazo ni dhaifu kifikra na mawazo mafupi. Sisi hatujifichi nyuma kwa maneno yasio na msimamo bali tunaimani juu ya uzito wa fikra na hoja zetu. Wanachama wetu wamefanya mijadala na baadhi ya wasomi wa kuu wa magharibi kama vile Naom Chomsky, Daniel Dennett and Flemming Larsen wa IMF, kwa sababu tunaamini ndio njia pekee ya maendeleo ya binaadamu kuwa na mijadala ya kimataifa na mazungumzo ya busara na hoja. Tunaamini kuwa muda wa kuitana “extremist” na “moderate” umepita na tunaamini kuwa upo uwezekano kwa watu wenye busara na hoja za kujadiliana kukaa pamoja na kujadiliana juu ya fikra na hoja wanazo linganiana kwa watu.
Kama utapendelea wanachama wetu kushiriki katika mijadala na maongezi ya busara ambayo munaandaa tafadhali wasiliana na sisi.
Je, Hizb ut-Tahrir inashirikiana na vyama vingine?
Hizb ut-Tahrir haina ushirika na wanaharakati au vyama vingine vyovyote vya Kiislam na visivyo kuwa vya Kiislam ikiwa kwa jina au vitendo.
Kwa nini Hizb ut-Tahrir kimefungiwa katika nchi nyingi?
Hizb ut-Tahrir ipo msitari wa mbele katika harakati za kisiasa katika nchi za Waisilam. Chama kimepingana na kuwakosowa viongozi wa ovu wote wa nchi za Waisilam duniani. Majibu ya uongozi wa nchi hizi juu ya harakati zetu ni kuwafunga, kuwatesa na kuwauwa wanachama wetu. Wakatika harakati zetu juu ya uongozi wa nchi hizi ni upinzani wa fikra na hoja za kisiasa kwa kuhamasisha majadiliano na maongezi ya busara, wao wamekimbilia kutufungia na kunyamazisha chama kama walivyo wao wenyewe kuwa na ukosefu wa hoja na fikra nzito. Kama kawaida ya uongozi wa nchi hizi zisizokubali upinzani wa aina yeyote, vyama vingine pia vimefungiwa. Licha ya kukifungia chama na vitisho dhidi ya wanachama, fikra na hoja za chama zimefanikiwa kufika katika jamii zote.
Ni nani anaye ifadhili Hizb ut-Tahrir?
Chama na shughuli zake zote zinafadhiliwa na wanaharakati wake wenyewe na hatupokei wala kukubali msaada wa aina yeyote kutoka katika serikali ya aina yoyote. Tangu harakati za Hizb ut-Tahrir zinategemea fikra na hoja, gharama za uendeshaji ni ndogo na fikra hazina gharama yoyote.
Ni nani kiongozi wa Hizb ut-Tahrir na yupo pahala gani?
Kiongozi mkuu wa Hizb ut-Tahrir anaitwa Ata Abu Rushta, yupo katika nchi ya Waisilam. Ni muandishi wa nyaraka na vitabu vingi vya kisiasa ya Kiisilam na sheria za Kiisilam, huko nyuma alikuwa mzungumzaji wa chama nchini Jordan. Wakati wa wakilishi wake wa chama kama mzungumzaji wa chama alikamatwa kwa miaka kadhaa kwa kosala kuwa na fikra na hoja kali dhidi ya utawala wa nchi. Tangu apewe uongozi wa chama amehutubia katika mihadhara mbali mbali kama Yemen, Pakistani na UK. Na ni mzungumzaji wa kawaida katika mtandao wa sauti ya Hizb ut-Tahrir Media Office, (http://www.hizb-ut-tahrir.info)/.
Kutokana na ukamatwaji na mateso wanayoyakabali wanachama wetu katika nchi za Waisilam na uongozi wao, hatutoi habari kamili kuhusu makaazi halisi ya uongozi wa chama.
Je, mtu yeyote anaweza kuhudhuria vikao vya Hizb ut-Tahrir?
Vikao vyetu vyote vinafanywa hadharani na mtu yeyote anakaribishwa kushiriki bila ya kujali fikra zake, siasa yake. Tunampa kila anaehudhuria haki ya kujadili juu ya mada ya mkutano bila ya kujali msimamo wake juu ya Uisilam au mada ya mkutano.
Ni upi msimamo wa Hizb ut-Tahrir juu ya matukio ya 9/11 na 7/7 na mauaji ya raia?
Sheria ya Kiisilam imekataza kabisa dhuluma juu ya raia. Sheria imekataza mauaji ya watoto, wazee na wanawake hata kwenye uwanja wa vita. Sheria zimekataza utekaji nyara wa ndege za abiria wasio na hatia na zimekataza uangamizaji wa majumba, maofisi ambazo zinatumiwa na raia wasio na makosa. Vitendo vyote hivi ni vitendo vya dhuluma ambavyo Uisilam vimekataza.
Ni upi mtazamo wa Hizb ut-Tahrir juu ya Demokrasia?
Mfumo wa Kiisilam wa utawala ni wa Khilafah ambao unaruhusu na kusisitiza ukosowaji wa kiongozi, uchaguwaji (kura) na kusikiliza maoni ya watu. Uisilam hauruhusu sera za nchi kuamuliwa na kuongozwa na mashirika tajiri au wafanya biashara wakubwa. Uisilam unawalazimisha wananchi wa Khilafah kushiriki katika siasa na kuukosoa uongozi wake.
Bila ya shaka Demokrasia katika nchi za Kibepari ni mfumo wa utawala ambao upo tofauti kabisa na mfumo wa utawala wa Kiisilam. Hii ni kwa sababu Uisilam na Ubepari zimejengeka kutoka katika misingi miwili tofauti. Mfumo wa Ubepari unalingania mamlaka ya utungaji sheria ni ya binaadamu, wakati mfumo wa Uisilam unalingani kuwa mamlaka ya utungaji sheria ni ya Muumba, Allah (swt). Kwa sababu hii, Demokrasia hailingani kabisa na mfumo wa Kiisilam.
Demokrasia inajulikana kwa uwazi kuwa ni mfumo wa wizi, ambao unamilikiwa na mashirika makubwa na upo mbali na mahitajia ya raia. Idadi ya wanaojitokeza kupiga kura katika nchi za Magharibi zimekuwa ndogo wakati wote na watu wanalazimika kuandamana kwa mamia na maelfu kuonesha hasira zao na uchofu wao wa maisha walionayo. Ijapo kuwa kila mmoja ana “uhuru” wa kukosoa na kubadilisha wanasiasa wao, ukweli ni kuwa yeyote wanaye mchagua ni mtumiwaji na mashirika tajiri makubwa na kiongozi anatawala kwa niaba ya mashirika hayo.
Kwa nini Hizb ut-Tahrir haishiriki kwenye Bunge/ baraza la Mawakilishi?
Uongozi unao tawala siku hizi katika nchi za Waisilam si uongozi wa Kiislam. Ni uongozi usio ongoza kwa mfumo wa Kiisilam, kwa sababu mfumo na sheria zao hazitoki katika Uisilam (isipokuwa baadhi ya sheria). Imekatazwa kwa Muisilam ambaye anaimani juu ya Uisilam, kusaidia, kushiriki au kuwa miongoni mwa uongozi huo. Hizb ut-Tahrir inawasisitiza Waisilam juu ya kufanya kazi kwa jitihada zao zote na kwa haraka kuziondosha tawala hizo na kusimamisha mfumo wa utawala wa Kiisilam badala yao.
Sisi hatukusidii kuwaongezea muda viongozi waovu na mifumo yao ya uongozi kwa kushrikiana nao.
Ukhalifah.
Nini Khilafah?
Khilafah inamaana ya mfumo wa utawala (uongozi) ambao umepatikana kutoka katika maandishi ya Kiisilam (Qur-an na Sunna). Unamajukumu yakusimamisha sheria za Kiisilam katika nyanja zote za maisha. Unatekeleza sheria zote zinazo husiana na mahakama, utawala, uchumi, kijamii, elimu na uhusiano na nchi za nje (foreign policy). Ukhalifah ni mfumo fofauti kulinganisha na mifumo mingine yote ya utawala kama demokrasia na ufalme.
Khilafah itachukuwa jukumu la kuleta mawasiliano baina ya Waisilam wote na utaondosha tofauti zote za kikabila na utaifa. Nchi ya Kiisilam si mali ya kabila fulani, chama fulani au watu wa namna fulani. Mtazamo wake juu ya raia wake, Waisilam na wasio kuwa Waisilam ni mmoja. Utafuata sheria ya Kiisilam wenye ushahidi uliomzito kutoka katika maandiko (Qur-aan na Sunna). Sio nchi ya jamii fulani au rangi fulani. Waarabu na wasio kuwa Waarabu, weupi na weusi wanahaki sawa mbele ya uongozi. Ijapokuwa Khilafah ni nchi ya Kiisilam, haiangalii masilahi ya Waisilam tu bali kila mmoja ambaye ni raia wa Khilafah, akiwa Muisilam na asie kuwa Muisilam. Utawala wa Kiisilam (Khilafah), unamajukumu ya kuwatimizia mahitaji yao raia wasio kuwa Waisilam kama raia na si kama jamii ndogo geni “ethinic minority”.
Upo wapi Ukhalifah leo?
Ukhalifah wa aina yeyote haupo duniani popote siku hizi. Ulipinduliwa wakati wa vita vikuu vya kwanza vya dunia na Mustafa Kemal wa Uturuki.
Kuelezea katika kuangushwa kwa Khilafah, Lord Curzon aliye kuwa sekeretari wa mambo ya nje wa Uengereza aliiambia Bunge “house of Common” tarehe 24th July 1924 kuwa “…Uturuki (kiti cha Khilafah) kimekufa na hakitorudi tena kwa sababu tumeutokomeza nguvu yake, Ukhalifah na Uisilam”.
Ni ipi nafasi ya mwanamke katika Khilafah?
Mwanamke atakuwa na nafasi zote chini ya uongozi wa Khilafah katika kuchangia maendeleo ya nchi kiuchumi, utajirisho, kielimu na technologia. Khilafah inawajibika kutoa elimu ya bure kwa wanaume na wanawake katika masomo ya primary na sekondari pia kutoa msaada wa bure kwa elimu ya juu katika vipengele vya madawa (medicine) na sayansi. Hii itawasaidia wanawake kupata kazi nzuri za kiujuzi kama matibabu (doctor), uinjinia, sayansi, architecture, uwalimu na zinginewe. Wanawake wataruhusiwa kufanya biashara, kujitajirisha, kuendesha biashara, kuajiri na kuajiriwa. Anaweza kwa mfano, kuajiriwa kama sekeretari (Administrative) wa serikali, au kuwa Jaji au kufanya pirika zote za kimaisha. Kwa kuongezea, pia atatimiza wajibu wake kama mke na mama, kujenga utulivu katika familia, kuwaangalia watoto wake na kujenga ufahamu muhimu wa kuendeleza kizazi cha kesho. Pia atakuwa na nafasi muhimu katika siasa na sauti nzito ya kisiasa juu ya kuukosoa uongozi kwa dhulma yoyote na kuwa makini juu mambo ya jamii yake.
Vipi wanaume na wanawake wataishi katika Khilafah?
Wanaume na wanawake watashirikiana ili kutimiza mahitaji yao ya jamii ndani ya mipaka ya mfumo wa jamii wa Kiisilam ambao umeweka sheria kuhusu uhusiano wa wanaume na wanawake. Hii inajenga mazingira yanayo ruhusu ushirikiano baina yao na unawawezesha wao kutimiza mahitaji yao ya kijamii na haki zao bila ya kuleta madhara katika nchi. Inahakikisha utu na uchi wa pande zote zimesitiriwa na kuwa uhusiano wa matamanio baina ya mwanaume na mwanamke upo ndani ya ndoa. Kwa mafano, Uisilam umeweka wazi vazi maalum la nje katika jamii kwa Muisilam mwanamke na pia lazimisha kuhifadhi yanaopendezesha mbele ya wanaume ambao wanao ruhusika kumuoa, na imekataza kukaa pahala pamoja wawili peke yao. Uisilam umekataza mchanganyiko baina ya wanume na wanawake au kitendo chochote kitakacho pelekea uzinifu. Mwanamke ni thamani inayotaka kutunzwa chini ya utawala wa Khilafah kwa hivyo hakuna kitendo chochote kitakacho ruhusiwa kufanyika ambacho kitahatarisha jambo hilo.
Vipi Khilafah itawaangalia wasio kuwa Waisilam?
Mwanazuoni mkubwa aitwae Imam Qarafi alisema “Ni wajibu wa Waisilam juu ya wasio kuwa Waisilam (Dhimma) kuwaangalia wliokuwa dhaifu miongoni mwao, kutimiza mahitaji ya masikini, kuwavisha, kuwalisha, malazi na kuongea nao kwa upole, na kuwakinga na mabalaa hata kama yatasababishwa na jirani aliyekuwa Muisilam. Waisilam ni lazima wawashauri kwa wema juu ya mahitaji yao na kuwakinga dhidi ya mtu yeyote ambaye atajaribu kuwadhuru wao na familia zao, kuiba mali zao au yeyote atakaye wadhulumu haki zao.”
Wengi wasio kuwa Waisilam waliwahi kuishi na Waisilam chini ya utawala wa Kiisilam kwa kipindi kisicho pungua karne kumi na tatu (13). Kwa muda wote huo walipewa haki sawa na Waisilam na maisha ya sawa kama ya Waisilam. Walikuwa na huduma sawa, furaha, utulivu na amani ya maisha yao.