Bismillah Ar-Rahmaan Ar-Raheem
Ilikuwa tarehe 3 mwezi wa March, 1924 alipotangaza myahudi na kibaraka wa waingereza, Mustafa Kamal (anayeitwa Ataturk) kuvunjwa kwa Khilafa kama nidhamu ya utawala—ambayo kutokamana kwayo
Waislamu walitawaliwa kwa karne kumi na tatu—na kubadilisha na nidhamu ya kikafiri ya kiilmaniyya kwa ajili ya kuanzisha zama ambapo Waislamu watarudi nyuma katika kubeba ulinganizi na kushindwa kutawala
mambo yao. Kwa hivyo wakawa ni ngawira za makafiri na wakagawanywa vipande vipande: biladi zao zikagawanywa, mali yao kuporwa, na viduduwatu wakapewa haki ya kuhukumu juu yao. Na idadi ya viongozi ambao makafiri waliowachagua kwa makini kuhudumia malengo yao waliongezeka. Wakauonjesha Umma kila aina ya tahayuri na fedheha, kuhukumu Umma na ukafiri wazi na kusalimisha mambo yao kwa mikono ya maadui…..mpaka mulipofika katika hali mwawaona maadui wenu wanavyowadharau na kualikana dhidi yenu, kufikia hadi ambayo mumerudi nyuma katika dini yenu ilhali munavamiwa katika nyumba zenu.
Kuvunjwa kwa Khilafa haikanza siku yahudi huyu (Ataturk) alipotangaza kuvunjwa kwake. Bali ilianza kutoka siku Waislamu walichanganyikiwa katika kufahamu dini yao, na kuanza kuingiza ndani yake fikra na hukmu zisizotokamana nayo na kubadilisha mwelekeo wao wa lugha ya kiarabu ambayo ni lugha ya Qur’an; na lugha zao zikaekwa mbali na lugha ya kiarabu na ufahamu wao ukaharibiwa. Kwa hivyo wakaanza kuchukuwa yale yanaogongana na ufahamu sawa au kila kilichowavutia kutokamana na fikra geni na matamanio yao. Kwa hivyo Umma ukakabiliwa na udhaifu katika kufahamu mfumo wao, mfumo ambao ndio msingi iliojengewa serikali ya Khilafa, na kudhoofika kwa kushindwa katika utabikishaji wake. Kwa hivyo natija yake ni kuwa nguzo za mwamko zikatingishwa na Khilafa kuvunjwa vipande vipande, kila kipande kupewa msimamizi aliyesimama kama mlinzi muaminifu kwa maslahi ya makafiri—ilhali akiwa ni khaini kwa dini yake na Umma—wanaowangojea kuwavamia.
Enyi Waislamu!
Mwajua ya kwamba Umma hautoweza kuinuka isipokuwa kwa kuufahamu mfumo wao vizuri na kuutabikisha kisawasawa. Kwa hivyo, je Umma utaweza kuufahamu vizuri mfumo wake ilhali baado yatukuza matamanio yake katika mas’ala ya kiSheria? Je, Umma utaweza kuwa na ufahamu sawa wa mfumo wake ilhali yakimbilia kumeza fikra za kikafiri mfano ya demokrasia na uhuru unaotakamana nayo? Au, je, utaweza kufahamu mfumo wake sawasawa pasina kutekeleza masharti yanaolazimika katika kuufahamu miongoni mwa lugha ya kiarabu na masomo ya dini? Na, je, Uislamu utaweza kutekelezwa pasina serikali ya Khilafa ambao kupitia kwake maisha ya Kiislamu yahuishwa pamoja
na kubeba ulinganizi wake kwa ulimwengu kupitia hoja na Jihad?
Kwa hivyo, twawalingania kwa ufahamu wazi wa Uislamu usiotatanisha, na kadhalika kusimamisha serikali ya Khilafa iliovunjwa na mkafiri. Kwa hivyo itikieni mwito wa yule anaewalingania kwa hukmu ya Allah, kwa sababu Allah amewaamrisha aliposema:-
وَأَنْ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ
“Hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Allah, wala usifuate matamanio yao na jitahadhari wasikufitinishe kutoka baadhi tu ya yale Allah aliyokuteremshia”[5:48]
Na Allah (swt) asema:-
وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الْكَافِرُونَ“Na yoyote asiehukumu kwa aliyo teremsha Allah, basi hao ndio makafiri” [5:44]
Kwa hivyo kimbilieni kwa utukufu na izza ya dunia na Akhera, na jikomboeni kutoka kutawaliwa na makafiri na kutoka fimbo yao wanayawapiga nayo nyusoni na migongoni. Na tarajieni siku za utukufu zinazokuja kwa sababu Allah ametuahidi msaada wake.
Allah (swt) asema:-
وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ
“Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini” [30:47]
Na Allah (swt) asema:-
وَلَيَنصُرَنَّ اللَّهُ مَنْ يَنصُرُهُ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ
“Na bila ya shaka Allah humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Allah ni Mwenye Nguvu Mtukufu” [22:40]
Na Hudheifa amepokea kutoka kwa Mtume wa Allah (saw) aliesema:
تكون النبوة فيكم ما شا ء الله أن تكون ثم يرفعها إذا شا ء أن يرفعها. ثم تكون خلآفة على منهاج النبوة فتكون ما شا ء الله أن تكون. ثم يرفعها إذا شاء الله أن يرفعها. ثم تكون ملكا عا ضا فيكون ما شاء الله أن يكون. ثم يرفعها إذاشاءالله يرفعها. ثم تكون ملكا جبرية فتكون ما شاء الله أن تكون ثم يرفعها إذاشاء الله أن يرفعها. ثم تكون خلآفة علي منهاج النبوة
“‘Utume utabakia miongoni mwenu mpaka Allah atakapopenda, kisha Allah atauondoa anapopenda.. Baadaye itakuja Khilafa kwa njia ya Utume na itabakia mpaka Allah atakapopenda, kisha Allah atauondoa anapopenda. Baadaye utakuja utawala wa kuumiza na utabakia mpaka Allah atakapopenda, kisha Allah atauondoa. Baadaye utakuja utawala wa ki-imla (udikteta) na utabakia mpaka Allah atakapopenda, kisha Allah atauondoa anapopenda. Baadaye itakuja Khilafa kwa njia ya Utume.’ Na hapa Mtume (saw) akanyamaza”.
Kwa hivyo jitoleeni kwa yale Allah aliyowaahidi na muliobashiriwa na Mtume, kwa sababu mutanali mafanikio ya dunia na Akhera kupitia hayo.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ
“Enyi mlio amini! Muitikieni Allah na Mtume anapo kuitieni kwa yanaowapa uzima wa milele. Na jueni kuwa Allah huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [8:24]